Madaktari nchini Sudan wafanya mgomo kulalamikia maslahi yao ya kazi
Madaktari nchini Sudan wamefanya mgomo kuishinikiza serikali ya nchi hiyo kuboresha maslahi yao ya kazi.
Mgomo huo ulioanza jana, umeitishwa na umoja wa madaktari wa nchi hiyo kwa lengo la kuitaka serikali kuongeza mishahara, marupurupu na kudhamini usalama wao wa kazi.
Umoja wa madaktari nchini Sudan umetangaza kuwa, katika kipindi cha mgomo huo madaktari hawatafanyakazi ila pale kunapotokea dharura.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, madaktari wa Khartoum, mji mkuu wa nchi hiyo na majimbo mengine ya Darfur kaskazini na magharibi, jimbo la Al Jazirah, katikati na kadhalika jimbo la Sennar, kusini mwa nchi hiyo, wamegoma kufanyakazi.
Kabla ya hapo madaktari wa nchi hiyo walilalamikia kiwango cha chini cha mshahara, huduma mbaya za hospitalini na kuongezeka vitendo vya ukandamizaji dhidi yao.