Maandamano ya wanachuo Afrika Kusini yashika kasi; polisi yaendelea kukabiliana nayo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i17149-maandamano_ya_wanachuo_afrika_kusini_yashika_kasi_polisi_yaendelea_kukabiliana_nayo
Maandamano ya wanachuo nchini Afrika Kusini yanaripotiwa kuongezeka baada ya baadhi ya vyuo kufunguliwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 10, 2016 10:49 UTC
  • Maandamano ya wanachuo Afrika Kusini yashika kasi; polisi yaendelea kukabiliana nayo

Maandamano ya wanachuo nchini Afrika Kusini yanaripotiwa kuongezeka baada ya baadhi ya vyuo kufunguliwa.

Mamia ya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Wits cha mjini Johannesburg leo wameandamana wakilalamikia sera za serikali katika kushughulia hali ya wanachuo.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, barabara za Chuo Kikuu cha Wits leo zimeshuhudia maandamano makubwa ambayo yameingiliwa kati na polisi na kupelekea kutokea vurugu kubwa.

Vitendo vya vyombo vya usalama vya Afrika Kusini vya kutumia mabavu dhidi ya maandamano ya amani ya wanachuo hao vinakithiri katika hali ambayo, masomo katika vituo vingi vya elimu na Vyuo Vikuu yamesimamishwa  katika mji wa Johannesburg.

Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Afrika Kusini wamekuwa wakifanya maandamano ya amani kwa muda sasa kulalamikia siasa za serikali ya Rais Jacob Zuma na mazingira yao ya masomo.

Polisi  wakikabiliana na maandamano ya wanachuo

Kilio kikubwa cha wanachuo hao ni ongezeko kubwa la karo na takwa lao la kuongezewa posho.

Hata hivyo maandamano hayo ya amani ya wanachuo yamekuwa yakizusha vurugo na fujo kati yao na vyombo vya usalama ambavyo vimekuwa vikitumia mabomu ya machozi na risasi za blastiki kuwatawanya wanachuo hao.

Mara kadhaa kumefanyika mazungumzo ya wakuu wa vyuo vikuu vya Afrika Kusini na wawakilishi wa vyama vya wanachuo lakini mazungumzo hayo yameshindwa kuzaa matunda.