Mlipuko wa Bomu waua watu Bujumbura, Burundi
Mlipuko uliotokea mapema leo mjini Bujumbura umeua mtu mmoja na kujeruhi wengine kadhaa.
Meya wa jiji la Bujumbura, Freddy Mbonimpa amesema mlipuko huo ambao umetokea katika soko la Kwa Siyoni, umeua mtu mmoja na kujeruhi wengine 7.
Mauaji hayo yametokea siku moja kabla ya safari ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon nchini Burundi katika jitihada za kukomesha mgogoro wa ndani na mauaji ya kiholela yanayoendelea hapa na pale nchini huko.
Jumapili ya jana pia watu wawili waliuawa katika shambulizi lililotokea katika eneo la Gisozi mkoani Mwaro katikati mwa Burundi. Mkuu wa mkoa huo, Jean-Marie Nyakarerwa amesema kuwa hii ni mara ya nne kwa watu wenye silaha kufanya mashambulizi mkoani humo katika kipindi cha wimbi mbili zilizopita.
Burundi ilitumbukia katika machafuko ya ndani baada ya kiongozi wa sasa wa nchi hiyo, Pierre Nkurunziza kutangaza nia yake ya kugombea urais kwa mara ya tatu mfululiizo Aprili mwaka jana..