Ushahidi waonesha: Ndege ya Misri iliangushwa na magaidi
(last modified Fri, 16 Dec 2016 03:49:55 GMT )
Dec 16, 2016 03:49 UTC
  • Ushahidi waonesha: Ndege ya Misri iliangushwa na magaidi

Kuna uwezekano mkubwa kwamba, ndege ya Misri iliyoanguka mapema mwa mwaka huu na kuua makumi ya watu ililipuliwa na magaidi.

Tuume ya uchunguzi iliyoundwa kufuatilia tukio la kuanguka ndege ya abiria aina ya Airbus ya Shirika la Ndege la Misri juu ya Bahari ya Mediterranean imetangaza kuwa, ndege hiyo ilikuwa na mada za milipuko.

Tume hiyo imetangaza katika ripoti yake kwamba, ripoti ya uchunguzi wa kitiba uliofanyika kwenye miili ya maiti za baadhi ya wahanga wa tukio hilo inaonesha kuwa, zilikuwa na mabaki ya mada za milipuko.

Ndege ya Shirika la Ndege la Misri

Ripoti hiyo inathibitisha kwamba, ndege hiyo ya abiria ilianguka kutokana na hujuma na kitendo cha uhalifu.

Ndege aina ya Airbus-A320 ya Shirika la Ndege la Misri iliyokuwa na abiria 66 ilianguka baharini Mei mwaka huu na kuua watu wote waliokuwemo baada ya kuondoka Paris, Ufaransa ikielekea Cairo.