Watunisia waandamana kuunga mkono mapinduzi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i23461-watunisia_waandamana_kuunga_mkono_mapinduzi
Maelfu ya wananchi wa Tunisia wamefanya maandamano leo katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo kuadhimisha mwaka wa 6 tangu wafanye mapinduzi yaliyoindoa madarakani serikali ya dikteta wa zamani wa nchi hiyo, Zainul Abidin bin Ali.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 14, 2017 09:23 UTC
  • Watunisia waandamana kuunga mkono mapinduzi

Maelfu ya wananchi wa Tunisia wamefanya maandamano leo katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo kuadhimisha mwaka wa 6 tangu wafanye mapinduzi yaliyoindoa madarakani serikali ya dikteta wa zamani wa nchi hiyo, Zainul Abidin bin Ali.

Maandamano hayo yamefanyika katika maeneo mbalimbali ya Tunisa hususan katika mkoa wa Sidi Buzeid  uliko magharibi mwa nchi hiyo na waandamanaji wamelaani kitendo cha kuruhusiwa magaidi kurejea nchini humo. 

Waandamanji hao walibeba picha za wanajeshi na askari usalama wa Tunisia waliouawa na makundi ya kigaidi na vilevile picha za uharibifu uliofanywa na magaidi katika nchi ya Syria na kutoa wito wa kuzuiwa magaidi hao kurejea nchini na kuvuliwa uraia. 

Vijana wengi wa Tunisia wamejiunga na makundi ya kigadi kama Daesh katika nchi za Iraq na Syria

Vilevile walibeba picha za Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel na Rais François Hollande wa Ufaransa na kuwataja kuwa ni waungaji mkono wa ugaidi. 

Watunisia hao walikuwa wakipiga nara za kulaani makundi ya kigaidi na kutoa wito wa mapambano na kukabiliana na watu wanaowatuma vijana wa Tunisia kwenda kupigana vita bega kwa bega na magaidi katika nchi za Syria na Iraq.