Machafuko ya karibuni Burundi, yalalamikiwa vikali
Machafuko ya hivi karibuni yaliyotokea nchini Burundi na kuendelea kuvunjwa haki za binadamu nchini humo yameendelea kulalamikiwa vikali.
Mtandao wa habari wa Africa Time umeripoti habari hiyo na kusema kuwa, taasisi isiyo ya kiserikali ya misaada ya kibinadamu na kupambana na mateso nchini Burundi imesema kuwa, kutiwa mbaroni maafisa wa kijeshi nchini Burundi kunafanywa mfululizo na maafisa wa taasisi ya usalama wa taifa ya nchi hiyo SNR na kwamba jambo hilo halikubaliki kabisa.
Shirika hilo lizilo la kiserikali la misaada ya kibinadamu na kupambana na ukandamizaji nchini Burundi limeongeza kuwa, watu wasiopungua 13 wameuawa katika machafuko ya mwezi huu wa Januari nchini Burundi.
Taasisi kama vile Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC na jumuiya nyingine muhimu za Afrika zinafanya juhudi za kutatua mgogoro wa Burundi ambao umepelekea raia wengi kuuawa na kuwa wakimbizi ndani na nje ya Burundi.
Hatua ya maelfu ya wakimbizi wa Burundi ya kukimbilia katika nchi jirani imesababisha matatizo mbalimbali ya kisiasa na kiuchumi kwa nchi hizo.