Jan 21, 2017 04:37 UTC
  • Waasi wa Uganda washambulia kijiji kaskazini mwa Kongo DR, wateka nyara raia

Waasi wa Uganda wameshambulia wakazi wa kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuteka nyara wakazi kadhaa wa kijiji hicho.

Kiongozi wa eneo la Dungu lililopo katika mkoa wa Haut-Uele, kaskazi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, amesema kuwa waasi hao wa Uganda wamewateka nyara raia 25 wa kijiji cha Nango. Ameongeza kuwa, baada ya waasi hao kuwateka nyara wakazi wa kijiji hicho, waliwalazimisha kubeba vitu walivyoviiba kijijini hapo.

Baadhi ya waasi huko Kongo DR

Kwa mujibun wa kiongozi wa eneo la Dungu, mwenyekiti wa kijiji cha Nango ni kati ya watu waliotekwa nyara katika tukio hilo na kwamba, shambulizi hilo limewatia wasi wasi wananchi. Kufuatia hali hiyo, kiongozi huyo amelitaka jeshi la serikali kuingilia kati haraka kwa lengo la kuzuia kujikariri vitendo hivyo sanjari na kuwaokoa mateka hao. Duru za kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimedokeza kuwa, tayari jeshi la serikali limeanzisha msako kwa ajili ya kuwaokoa raia hao. Maeneo ya mashariki na kaskazini mashariki mwa Kongo DR yamekuwa yakishuhudia hali ya mchafukoge kwa miaka 20 sasa, kutokana na udhaifu wa askari wa serikali na wale wa kusimamia amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo.

Tags