SAUTI: Askari 850 wa Burundi watatumwa CAR wiki hii
Jan 23, 2017 13:13 UTC
Wanajeshi wapatao 188 wa Burundi wameelekea Jamuhuri ya Afrika ya Kati kujiunga na kikosi cha kofia ya buluu cha Umoja wa Mataifa cha kusimamia amani nchini humo.
Kwa kipindi cha wiki moja jumla ya askari 850 wa nchi hiyo, wataelekea huko kuchukua nafasi ya askari wenzao waliohudumu katika kikosi hicho kwa zaidi ya miezi 18 bila kubadilishwa.
Hii ni katika hali ambayo awali kulienea habari za uwezekano wa askari wa Burundi kutimuliwa Jamhuri ya Afrika ya Kati hasa baada ya kushadidi mvutano wa kisiasa nchini Burundi.
Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Bujumbura Hamida Issa kwa taarifa kamili.............../
Tags