Umoja wa Mataifa watahadharisha kuhusu njaa na ukame nchini Burundi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i24249-umoja_wa_mataifa_watahadharisha_kuhusu_njaa_na_ukame_nchini_burundi
Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusu ukame na njaa inayotishia nchi ya Kiafrika ya Burundi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 26, 2017 00:11 UTC
  • Umoja wa Mataifa watahadharisha kuhusu njaa na ukame nchini Burundi

Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusu ukame na njaa inayotishia nchi ya Kiafrika ya Burundi.

Mfuko wa Idadi ya Watu wa Umoja wa Mataifa (UNFPA) umetangaza katika ripoti yake kwamba, raia milioni tatu wa Burundi ambao ni sawa na robo ya wakazi wa nchi hiyo wanahitaji msaada wa haraka wa chakula na huduma nyingine muhimu za kukidhi mahitaji yao.

Aidha ripoti hiyo inasema kuwa, wimbi la lishe duni na vifo vinavyosababishwa na tatizo hilo si jambo la kufumbia macho.

Sehemu nyingine ya ripoti ya Mfuko wa Idadi ya Watu wa Umoja wa Mataifa (UNFPA) inaeleza kuwa, licha ya viongozi wa serikali ya Burundi kuwazuia wanahabari wa kigeni kuripoti kuhusu hali ya mambo ya nchi hiyo na kutoa habari zinaoonyesha kuboreka hali ya usalama na ya kimaisha katika nchi hiyo, lakini matamshi hayo ya viongozi wa serikali ya Bujumbura yako mbali kabisa na ukweli wa mambo.

Wakimbizi wa Burundi

Burundi ilitumbukia katika machafuko mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka 2015 baada ya chama tawala cha CNDD-FDD kumuidhinisha Rais Pierre Nkurunziza, kugombea urais katika uchaguzi mkuu uliopita, machafuko ambayo yalishika kasi zaidi mjini Bujumbura.

Ripoti mbalimbali zinaonyesha kuwa, zaidi ya raia 400 wameuawa nchini Burundi tangu nchi hiyo ilipotumbukia katika machafuklo huku Umoja wa Mataifa ukisema kuwa, raia laki tatu na 20 elfu wameikimbia Burundi tangu wakati huo na kuomba hifadhi katika nchi jirani.