Ukiukaji wa haki za binadamu waongezeka huko nchini Sudan Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i26438-ukiukaji_wa_haki_za_binadamu_waongezeka_huko_nchini_sudan_kusini
Umoja wa Mataifa umetahadharisha kwa mara nyingine tena kuhusu kuongezeka ukiukaji wa haki za binadamu katika nchi iliyokumbwa na vita ya Sudan Kusini.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 16, 2017 00:31 UTC
  • Ukiukaji wa haki za binadamu waongezeka huko nchini Sudan Kusini

Umoja wa Mataifa umetahadharisha kwa mara nyingine tena kuhusu kuongezeka ukiukaji wa haki za binadamu katika nchi iliyokumbwa na vita ya Sudan Kusini.

Yasmin Suka, Mkuu wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini amesema kuwa, athari za maafa na hususan vitendo vya ubakaji inavayofanywa huko Sudan Kusini ni vya kuogofya na kwamba upuuzaji wa jamii ya kimataifa kwa suala hilo huwenda ukasababisha maangamizi ya kizazi na kupotea watu wengi nchini humo. 

Yasmin Suka ameongeza kuwa, serikali ya Sudan Kusini na vikosi vitiifu kwa serikali hiyo huwatumia kijeshi raia kwa makusudi na kuwalenga kwa mashambulizi kutokana na sababu za kikabila.  

Vikosi vitiifu kwa serikali ya Sudan Kusini

Wakati huo huo John Luk Jok, Waziri wa Sheria wa Sudan Kusini amepinga ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa na kuwataja wanamgambo wa upinzani kuwa ndio wanaohusika na maafa hayo huko Sudan Kusini. Mapigano katika maeneo mbalimbali huko Sudan Kusini hadi sasa yamesababisha kuuliwa watu karibu laki moja na nusu. Mbali na kuathiriwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, Sudan Kusini inakabiliwa pia na matatizo mengine kama njaa na magonjwa mbalimbali ya kuambukiza, huku raia wa nchi hiyo karibu milioni sita wa maeneo ya kusini mwa nchi hiyo wakikabiliwa na njaa kubwa.