Mchakato wa kisiasa Burundi wazidi kugonga mwamba
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i28232-mchakato_wa_kisiasa_burundi_wazidi_kugonga_mwamba
Burundi inaelekea kuathiriwa tena na mgogoro wa kisiasa licha kufanyika juhudi za kikanda na kimataifa za kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 25, 2017 03:49 UTC
  • Mchakato wa kisiasa Burundi wazidi kugonga mwamba

Burundi inaelekea kuathiriwa tena na mgogoro wa kisiasa licha kufanyika juhudi za kikanda na kimataifa za kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo.

Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa, mgogoro wa kisiasa Burundi ambao ulianza kufuatia uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo wa kusalia madarakani kwa muhula wa tatu mfululizo, umesababisha vifo vya watu elfu mbili, mamia ya wengine kutoweka na maelfu kuwa wakimbizi katika nchi jirani. 

Wakimbizi wa Burundi waliokimbia machafuko nchini kwao 

Benjamin Mkapa, Rais mstaafu wa Tanzania ambaye ni msuluhishi katika mgogoro wa kisiasa wa Burundi, ameshindwa kuandaa mazingira ya kufanyika mazungumzo kati ya serikali na wapinzani licha ya kupita miezi kadhaa hadi sasa, huku mashinikizo ya kimataifa kwa serikali ya Burundi yakisalia bila kuzaa matunda.

Leo Jumanne tarehe 25 Aprili ni siku ya kukumbuka kutumia mwaka wa pili tangu kuanza mgogoro wa kisiasa huko Burundi.