Zuma: Afrika Kusini inaondokana na mdodoro wa uchumi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i30928-zuma_afrika_kusini_inaondokana_na_mdodoro_wa_uchumi
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amesema kuwa nchi hiyo hivi sasa inaondoka katika hali ya mdodoro wa kiuchumi.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Jun 24, 2017 23:56 UTC
  • Zuma: Afrika Kusini inaondokana na mdodoro wa uchumi

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amesema kuwa nchi hiyo hivi sasa inaondoka katika hali ya mdodoro wa kiuchumi.

Rais Zuma ambaye jana alikuwa akihutubia bunge ameeleza kuwa uchumi wa Afrika Kusinihivi karibuni unatarajiwa kuondokana na hali ya kudorora;  hali ambayo iliathiri sekta  hiyo tangu mwezi Juni mwaka huu. Tangu miaka minane iliyopita hadi hivi sasa, hii ni mara ya kwanza uchumi wa Afrika Kusini unakumbwa na hali ya mdodoro. Rais Zuma amekiri kwamba hali hiyo imeitia wasiwasi mkubwa serikali yake. 

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini akihutubia bungeni 

Hii ni mara ya kwanza uchumi wa Afrika Kusini unaathiriwa na hali ya mporomoko tangu mwaka 2009 hadi sasa. Katika mwaka huo  uchumi wa Afrika kusini ulishuka  kufuatia kuwepo pia mgogoro wa fedha kimataifa. Hata hivyo Rais wa Afrika Kusini sasa anasema kuwa anatumai kwamba nchi yake itaondokana na hali hiyo haraka iwezekanavyo. 

Chama cha Congresi ya Taifa (ANC ) ambacho ni chama tawala nchini Afrika Kusini  kilichukua madarakani tangu mwaka 1994 yaani kuanzia mwaka ule ambapo mfumo wa ubaguzi wa rangi nchini humo (Apartheid) ulihitimishwa rasmi, hata hivyo kwa kuzingatia kufeli kwa sekta ya uchumi ya nchi hiyo,  chama hicho kimepoteza pakubwa uungaji mkono  wa wananchi.