Rais Nkurunziza wa Burundi apokea vitambulisho vya balozi mpya wa Iran
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i31216-rais_nkurunziza_wa_burundi_apokea_vitambulisho_vya_balozi_mpya_wa_iran
Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi amepokea vitmabulisho vya Murtadha Murtadhawi, Balozi mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye si mkazi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 01, 2017 23:44 UTC
  • Rais Nkurunziza wa Burundi apokea vitambulisho vya balozi mpya wa Iran

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi amepokea vitmabulisho vya Murtadha Murtadhawi, Balozi mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye si mkazi.

Kwa mujibu wa Shirika Rasmi la Habari la Iran, IRNA, Rais Nkurunziza  amefanya mazungmzo na Murtadhawi ambaye amemkabidhi rais huyo wa Burundi salamu za Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Katika mazungumzo hayo, Rais Nkurunziza amesema nchi yake inataka kuimarisha uhusiano na Iran katika nyanja zote ikiwa ni pamoja na kutembeleana maafisa wa ngazi za juu za nchi mbili. Halikadhalika amesisitiza kuhusu ulazima wa kutekelezwa mapatano ya nchi mbili katika uga wa kustawisha uhusiano  na uwekezaji wa mashirika ya Iran nchini Burundi.

Kwa upande wake Balozi Murtadhawi amepongeza ushirikiano mzuri wa Jamhuri ya Burundi na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mashirika ya kimataifa.

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia amemfahamisha Rais Nkurunziza kuhusu mwaliko rasmi wa kuitembelea Iran kutoka kwa Rais Hassan Rouhani kwa ajili ya kushiriki katika sherehe za kuapishwa rais Rouhani katika kipindi chake cha pili zitakazofanyika mwezi Agosti 5.

Aidha balozi wa Iran amemfahamisha Rais Nkurunziza kuhusu uwezo wa mashirika ya Kiirani katiak sekta mbali mbali na ulazima wa nchi mbili kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi.