FAO yatahadharisha kuhusu kuongezeka haja ya misaada ya dharura mashariki mwa Afrika
(last modified Mon, 24 Jul 2017 07:04:58 GMT )
Jul 24, 2017 07:04 UTC
  • FAO yatahadharisha kuhusu kuongezeka haja ya misaada ya dharura mashariki mwa Afrika

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetahadharisha katika ripoti yake kuwa kuna ongezeko la kutia wasiwasi la watu wanaohitaji misaada ya haraka ya kibinadamu katika nchi za mashariki mwa Afrika.

Dominique Burgeon Mkurugenzi wa Kitengo Kinachohusika na Hali za Dharura katika Shrika la FAO amesema kuwa kupungua kiwango cha mvua hivi karibuni katika maeneo ya mashariki mwa Afrika kumeathiri uzalishaji wa mazao ya chakuka na maisha ya familia mbalimbali katika eneo hilo na kwamba idadi ya watu wanaohitaji misaada ya kibinadamu ya kimataifa imeongezeka. 

Wakulima wa Ethiopia wakipanda mazao licha ya kukabiliwa na upungufu mkubwa wa mvua 

Dominique Burgeon ameongeza kuwa kupungua kiwango cha kunyesha mvua katika maeneo ya mashariki mwa Afrika yakiwemo pia maeneo ya kusini na katikati mwa Somalia, kusini mashariki mwa Ethiopia, kaskazini mashariki mwa Kenya, kaskazini mwa Tanzania, kaskazini mashariki na kusini mashariki mwa Afrika kumeshuhudiwa waziwazi na kwamba kulikuwa chini ya asilimia 50 pia ikilinganishwa na misimu iliyopita.

Shirika la FAO limeongeza kuwa watu milioni kumi na sita katika nchi tano za Somalia, Ethiopia, Kenya, Tanzania na Uganda pia wanahitaji msaada wa haraka wa chakula; kiwango ambacho kinatajwa kuongezeka kwa karibu asilimia 30 kuanzia mwishoni mwaka jana wa 2016. 

Tags