Baraza la Usalama lataka kufanyika uchaguzi wa Rais Kongo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i32324-baraza_la_usalama_lataka_kufanyika_uchaguzi_wa_rais_kongo
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ichukue hatua ya kuhakikisha kuwa uchaguzi wa Rais unafanyika nchini humo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 27, 2017 03:05 UTC
  • Baraza la Usalama lataka kufanyika uchaguzi wa Rais Kongo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ichukue hatua ya kuhakikisha kuwa uchaguzi wa Rais unafanyika nchini humo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeeleza kutiwa wasiwasi na mwenendo wa kinyonga wa makubaliano yaliyofikiwa nchini humo kwa ajili ya kuendesha uchaguzi wa Rais na kutahadharisha kuwa kushindwa kutekelezwa muafaka huo kutazidisha hatari ya machafuko na ukosefu wa amani nchini humo na katika eneo zima kwa ujumla.  

Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tarehe 7 mwezi huu alitangaza kuwa haiwezekani uchaguzi wa rais wa  nchi hiyo ukafanyika hadi kufikia mwezi Disemba mwaka huu. Mgogoro wa kisiasa nchini Kongo ulianza kufuatia kuakhirishwa tarehe ya kufanyika uchaguzi wa Rais na vile vile sisitizo la Rais Joseph Kabila la kusalia madarakani.  

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambaye anatajwa kuwa kiini cha mgogoro wa kisiasa nchini humo

Inaonekana kuwa ni jambo lisilowezekana kufanyika uchaguzi wa Rais huko Kongo licha ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya wapinzani na serikali ya Kinshasa ambayo yaliainisha tarehe 31 Disemba kuwa siku ya kufanyika uchaguzi wa Rais.