Uganda yatiwa wasiwasi na mlipuko wa virusi vya Marburg
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i35889-uganda_yatiwa_wasiwasi_na_mlipuko_wa_virusi_vya_marburg
Uganda imekumbwa tena na wasiwasi baada ya watu wawili kuripotiwa kufariki dunia kwa ugonjwa wa Marburg.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 23, 2017 04:39 UTC
  • Uganda yatiwa wasiwasi na mlipuko wa virusi vya Marburg

Uganda imekumbwa tena na wasiwasi baada ya watu wawili kuripotiwa kufariki dunia kwa ugonjwa wa Marburg.

Watu wawili wanaripotiwa kufariki dunia nchini Uganda tangu mwezi Septemba uliopita, kutokana na virusi hivyo vinavyoua kwa haraka kama virusi vya Ebola, hali ambayo imezusha wasiwasi mkubwa miongoni mwa raia wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Waziri wa Afya wa Uganda Dakta Jane Ruth Aceng amethibitilisha kufariki  dunia watu wawili kutokana na virusi vya Marburg nchini humo. Idara ya utafiti wa virusi vya Marburg nchini Uganda imesema kuwa, ugonjwa huo unaua haraka kama Ebola.

Ni homa inayosababisha mgonjwa kutokwa na damu, kutapika na kuharisha na ugonjwa wenye kuambukiza haraka. 

Wizara ya Afya nchini Uganda imeonya dhidi ya mlipuko wa virusi vikali vinavyosababisha ugonjwa wa Marburg katika eneo la Kusini Magharibi mwa nchi.

Dr. Jane Ruth Aceng, Waziri wa Afya wa Uganda

Katika taarifa ya wizara hiyo, maafisa wamesema kuwa uchunguzi wa maabara ulithibitisha kuwa watu wawili wa familia moja walifariki kutokana na virusi hivyo wilayani Kabale.

Virusi vya Marburg vinaweza kumuuwa mtu mwenye afya katika kipindi cha wiki moja tu baada ya kuanza kutapika na kuwa na kuharisha na hatimaye kutokwa damu ndani kwa ndani. Ugonja huo bado hauna tiba.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeeleza kuwa limetuma maafisa nchini Uganda ili kuimarisha juhudi za kuzuia mlipuko wa homa hiyo. Uganda imeshawahi kukumbwa na milipuko ya homa ya Ebola na Marburg katika siku za nyuma, japokuwa milipuko hiyo kwa kiasi kikubwa ilizuiwa kuenea haraka na hivyo kuzuia kusababisha maafa makubwa.