Wapinzani nchini Kongo wataka kuachiliwa huru wafungwa wa kisiasa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i35895-wapinzani_nchini_kongo_wataka_kuachiliwa_huru_wafungwa_wa_kisiasa
Wapizania wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wametangaza kuwa, karibu wafungwa 50 wa kisiasa wa upande wa upinzani, wanaendelea kushikiliwa katika korokoro za nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 23, 2017 10:34 UTC
  • Wapinzani nchini Kongo wataka kuachiliwa huru wafungwa wa kisiasa

Wapizania wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wametangaza kuwa, karibu wafungwa 50 wa kisiasa wa upande wa upinzani, wanaendelea kushikiliwa katika korokoro za nchi hiyo.

Danny Kabongo, Mkuu wa Umoja wa Vijana kwa ajili ya Demokrasia na Ustawi wa Kijamii nchini humo amesema kuwa, wapinzani wanaoendelea kushikiliwa ni wanaharakati wa kisiasa wa umoja huo  na kuitaka serikali ya Kinshasa kuwaachilia huru bila ya masharti yoyote. Kabongo ameongeza kuwa, watu hao walitiwa nguvuni na polisi mjini Lubumbashi wakati walipokuwa wameenda kukutana na Félix Tshisekedi, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Felix Tshisekedi, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Kongo DR

Aghlabu ya wafungwa wa kisiasa nchini humo walitiwa mbaroni baada ya kuendesha maandamano ya kupinga mabadiliko ya katiba yaliyokuwa na lengo la kuondoa ukomo wa muhula wa uongozi kwa rais hapo mwaka 2015. Kuanzia wakati huo, kamatakamata hiyo iliendelea hadi mwaka jana 2016 ambapo wapinzani kadhaa wa serikali walitiwa nguvuni. Hii ni katika hali ambayo serikali imekadhibisha habari ya uwepo wa wafungwa wa kisiasa katika jela zake na badala yake imesema kuwa, wafungwa hao wanashikiliwa kwa makosa ya jinai.