Magaidi wa al Shabab wateka mji wa Rassadi kusini mwa Somalia
(last modified Wed, 01 Nov 2017 08:21:09 GMT )
Nov 01, 2017 08:21 UTC
  • Magaidi wa al Shabab wateka mji wa Rassadi kusini mwa Somalia

Kundi la kigaidi la al Shabab limeuteka mji wa Rassadi ulioko kusini mwa Somalia baada ya askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika kuondoka katika eneo hilo.

Wapiganaji wa kundi la al Shabab waliuteka mji huo jana bila ya upinzani wowote na hadi sasa hakujatolewa sababu ya kuondoka askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika katika mji huo. 

Kabla ya tukio hilo askari kumi wa kikosi  cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika walikuwa wameuawa katika mlipuko wa bomu huko kaskazini mwa Somalia. 

Katika siku za hivi karibuni kundi la kigaidi la al Shabab limezidisha mashambulizi ya kujilipua kwa mabomu likiwemo lile lililoua watu wasiopungua 29 mjini Mogadishu siku kadhaa zilizopita.

Rais Mohamed Abdullahi Farmajo wa Somalia

Rais Mohamed Abdullahi Farmajo wa Somalia ametangaza azma ya serikali yake ya kupambana na magaidi katika nchi hiyo ambayo wiki za hivi karibuni imepoteza mamia ya raia katika mashambulio ya al Shabab. 

Akizungumza Jumatatu wakati wa kongamano la usalama, alisema lazima kuwepo mpango maalumu wa kuunganisha vikosi vya jeshi kote nchini Somalia ili kaungamiza magaidi wakufurishaji wa al-Shabab. 

Tags