OCHA: Wakimbizi wa Kongo DR wamekubwa na mgogoro mkubwa wa kibinaadamu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i36125-ocha_wakimbizi_wa_kongo_dr_wamekubwa_na_mgogoro_mkubwa_wa_kibinaadamu
Msemaji wa Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) ametahadharisha juu ya hali mbaya ya kibinaadamu inayowakabili wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 03, 2017 01:03 UTC
  • OCHA: Wakimbizi wa Kongo DR wamekubwa na mgogoro mkubwa wa kibinaadamu

Msemaji wa Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) ametahadharisha juu ya hali mbaya ya kibinaadamu inayowakabili wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Yvon Edoumou sambamba na kutahadharisha juu ya mgogoro huo wa kibinaadamu amesema kuwa, misaada michache ya kifedha ya wafadhili na wanaharakati wa masuala ya binaadamu kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, haiendani na ukubwa wa mahitaji ya wakimbizi wa nchi hiyo.

Makundi ya waasi yanayochafua usalama wa nchi hiyo ya katikati mwa Afrika

Kwa mujibu wa Edoumou, wakimbizi hao wanakabiliwa na matatizo mengi ambayo yanahitajia msaada zaidi wa kifedha. Msemaji wa Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa viongozi wa serikali ya Kinshasa, hawako tayari kutoa ushirikiano kwa ajili ya kuhitimisha matatizo hayo ya wakimbizi kama ambavyo pia wamefikia kuweka vizuizi katika ufikishaji misaada kwa walengwa, ingawa amesema kuwa mazungumzo ndio yanayoweza kusaidia kutatuliwa suala hilo.

Maisha ya raia wa Kongo DR yalivyo kwa sasa

Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, karibu watu milioni nne raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekuwa wakimbizi kutokana na machafuko yanayoendelea nchini mwao. Mbali na hayo ni kwamba karibu watu laki tano kutoka Burundi, Rwanda, Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati walikimbilia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na machafuko yanayotokea nchini mwao.