Tume ya Uchaguzi DRC yatangaza uchaguzi kufanyika Disemba 2018
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i36199-tume_ya_uchaguzi_drc_yatangaza_uchaguzi_kufanyika_disemba_2018
Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (CENI) imetangaza Jumapili kuwa uchaguzi wa rais atakayechukua nafasi ya Rais Joseph kabila utafanyika Disemba 23, mwaka ujao wa 2018.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Nov 06, 2017 05:43 UTC
  • Tume ya Uchaguzi DRC yatangaza uchaguzi kufanyika Disemba 2018

Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (CENI) imetangaza Jumapili kuwa uchaguzi wa rais atakayechukua nafasi ya Rais Joseph kabila utafanyika Disemba 23, mwaka ujao wa 2018.

Mkuu wa tume hiyo, Corneille Nangaa amewaambia waandishi habari mjini Kinshasa kuwa watu 43 milioni wamesajiliwa kama wapiga kura nchini humo hadi sasa.

Amesema matokeo ya uchaguzi huo yatatangazwa Januari 9 , 2019 na rais kuapishwa Januari 13.

Uchaguzi huo ulikuwa umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka 2016 na umeakhirishwa mara kadhaa.

Mgogoro wa kisiasa unaendelea nchini DR Congo, huku maandamano makubwa yakiendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini humo. Mapema wiki hii maandamano makubwa yakumshinikiza Rais Kabila kuaanda ucahguzi mwaka huu yalifanyika katika mji wa Goma, na siku baadae mjini Bukavu mashariki mwa nchi hiyo.