Tahadhari ya kuuawa wanajeshi zaidi kaskazini mashariki mwa DRC
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i36447-tahadhari_ya_kuuawa_wanajeshi_zaidi_kaskazini_mashariki_mwa_drc
Mkuu wa jumuiya moja ya kijamii ya kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ametahadharisha kuhusu kuongezeka mauaji ya wanajeshi wa nchi hiyo wanaouliwa na waasi.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Nov 17, 2017 00:42 UTC
  • Jeshi la Polisi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
    Jeshi la Polisi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Mkuu wa jumuiya moja ya kijamii ya kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ametahadharisha kuhusu kuongezeka mauaji ya wanajeshi wa nchi hiyo wanaouliwa na waasi.

Gyli Gotabo, mkuu ya jumuiya ya kijamii ya eneo la Irumu mkoani Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ametoa tahadhari hiyo na kuongeza kuwa, karibu wanajeshi 10 wa serikali wameuawa katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita baada ya kushambuliwa na waasi wa FRPI.

Hata wanawake wamejiunga na makundi ya waasi DRC

 

Duru za kijeshi mkoani Ituri zinasema kuwa, idadi ya wanajeshi wa serikali wanaouawa imeongezeka katika eneo hilo kutokana na wakazi wake kushirikiana na waasi.

Mkuu wa jumuiya hiyo ya kijamii amewataka wakazi wa eneo la Irumu kushirikiana na jeshi katika kutoa taarifa za maficho ya waasi hao.

Gyli Gotabo vile vile amelitaka jeshi la serikali kutowakandamiza waasi wanaojisalimisha na kuweka chini silaha zao.

Maeneo ya mashariki na kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamekuwa uwanja wa mapigano na mauaji kwa miaka 20 sasa.

Kushindwa jeshi la serikali na askari wa kofia buluu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa kukabiliana vilivyo na waasi ni moja ya sababu kuu za kupotea utulivu na amani katika maeneo hayo kwa miaka 20 sasa.