Serikali ya Congo DR yapiga marufuku maandamano ya wapinzani
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i36857-serikali_ya_congo_dr_yapiga_marufuku_maandamano_ya_wapinzani
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imepiga marufuku maandamano ya kambi ya upinzani yaliyopangwa kufanyika tarehe 30 mwezi huu wa Novemba kumshinikiz Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo aondoke madarakani.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Nov 27, 2017 04:40 UTC
  • Serikali ya Congo DR yapiga marufuku maandamano ya wapinzani

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imepiga marufuku maandamano ya kambi ya upinzani yaliyopangwa kufanyika tarehe 30 mwezi huu wa Novemba kumshinikiz Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo aondoke madarakani.

Serikali ya Kinshasa imechukua uamuzi huo licha ya wito wa jamii ya kimataifa unaoitaka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuheshimu haki za kidemokrasia na za kiraia nchini humo. 

Kambi ya upinzani Congo DR inapinga uamuzi wa serikali ya nchi hiyo wa kuakhirisha zoezi la uchaguzi wa rais uliokuwa umepangwa kufanyika tarehe 23 mwezi ujao wa Disemba na inamtaka Rais Joseph Kabila ang'atuke madarakani. Kambi hiyo imewataka wananchi kufanya maandamano kote nchini humo na kusisitiza kwamba, uchaguzi mkuu unapaswa kufanyika katika wakati ulioainishwa.

Kwa uapande wake serikali ya Kinshasa imetishia kuwa itatumia mabavu kukabiliana na waandamanaji.

Rais Joseph Kabila anatakiwa kung'atuka madarakani

Awali uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ulipangwa kufanyika Novemba mwaka 2016 lakini serikali ya Kinshasa iliahirisha zoezi hilo kwa kisingizio kwamba haikuwa na wakati wa kutosha wa kuandikisha majina ya wapigaji kura. Hata hivyo Tume ya Uchaguzi ya Congo imeahirisha tena zoezi hilo ikisema haiwezekani kuitisha uchaguzi wa rais kufikia mwishoni mwa mwaka huu.