Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) walaani shambulio la wanamgambo mashariki mwa Kongo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i37279-madaktari_wasio_na_mipaka_(msf)_walaani_shambulio_la_wanamgambo_mashariki_mwa_kongo
Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) imelaani shambulio lililofanywa na wanamgambo katika kituo chao kilichopo Masisi mkoani Kivu ya Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 06, 2017 22:11 UTC
  •  Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) walaani shambulio la wanamgambo mashariki mwa Kongo

Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) imelaani shambulio lililofanywa na wanamgambo katika kituo chao kilichopo Masisi mkoani Kivu ya Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mwakilishi wa Jumuiya hiyo ya Madaktari Wasio na Mipaka huko Kivu ya Kaskazini amelaani shambulio hilo la watu wenye silaha katika kituo chao na akasema kuna ulazima wa kutiwa mbaroni na kuhukumiwa wahusika wa shambulio hilo. 

Anna Halford amesisitiza kuwa Jumuiya ya MSF ni chombo kinachojishughulisha na huduma za kibinadamu kama vile utoaji wa huduma za afya na tiba katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini.

Madaktari wa Jumuiya ya MSF wakitoa huduma ya upasuaji kwa mama mjamzito huko Masisi nchini Kongo 

Amesema kuendelea mashambulizi kama hayo kunatia wasiwasi na ametaka kuungwa mkono taasisi hiyo na viongozi wa eneo. Wafanyakazi wawili wa MSF juzi Jumanne walitekwanyara na watu wenyesilaha walioshambulia kituo chao huko Masisi mkoani Kivu ya Kaskazini. Ni vyema kuashiria hapa kuwa watu 450,000 katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hawana huduma za afya na tiba kwa muda wa miezi minne sasa.