Waislamu Afrika Kusini wawaandalia Wakristo karamu kwa mnasaba wa Krismasi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i37999-waislamu_afrika_kusini_wawaandalia_wakristo_karamu_kwa_mnasaba_wa_krismasi
Waislamu na Wakristo wa mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini wamefanya kikao cha pamoja kwa mnasaba wa kuadhimisha na kukumbuka tukio la kuzaliwa Nabii Issa Masiih (as).
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 23, 2017 23:56 UTC
  • Waislamu Afrika Kusini wawaandalia Wakristo karamu kwa mnasaba wa Krismasi

Waislamu na Wakristo wa mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini wamefanya kikao cha pamoja kwa mnasaba wa kuadhimisha na kukumbuka tukio la kuzaliwa Nabii Issa Masiih (as).

Kikao hicho kilichofanyika kwa siku ya tatu mfululizo kimesimamiwa na msikiti wa kitongoji cha Wynberg mjini Cape Town kwa ajili ya karamu na dhifa kwa ajili ya Wakristo wa eneo hilo kwa mnasaba wa kukumbuka tukio la kuzaliwa Nabii Issa Masiih (as).

Vikao hivyo vinafanyika kwa lengo la kuimarisha mazungumzo baina ya dini mbalimbali na kujenga uwiano na mlingano wa kijamii. 

Sherehe hizo zimejumuisha hafla ya usomaji wa mashairi, maombi na dua na filamu zinazohimiza masuala yanayowakutanisha pamoja wafuasi wa dini mbili za Uislamu na Ukristo.

Afrika Kusini ina Waislamu karibu milioni moja, na asilimia 80 ya watu wa jamii ya nchi hiyo ni Wakristo. 

Wakristo kote duniani wanaadhimisha siku ya kuzaliwa Nabii Issa Masiih (as) tarehe 25 mwezi huu wa Disemba.