Kenya yajiunga na Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia AIIB
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i44056-kenya_yajiunga_na_benki_ya_uwekezaji_wa_miundombinu_ya_asia_aiib
Kenya imejiunga na na Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia AIIB ikiwa ni katika jitihada za nchi hiyo kutafuta fursa mpya za kuijiimarisha kiuchumi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 04, 2018 23:34 UTC
  • Kenya yajiunga na Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia AIIB

Kenya imejiunga na na Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia AIIB ikiwa ni katika jitihada za nchi hiyo kutafuta fursa mpya za kuijiimarisha kiuchumi.

Kenya imejiunga na Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia AIIB ikiwa ni katika jitihada za nchi hiyo kutafuta fursa mpya za kuijiimarisha kiuchumi.

Taarifa zinasema katika kikao chake wiki hii benki hiyo imepitisha azimio na kuafiki uanacama wa nchi mbili mpya ambazo ni Kenya na Papua New Guinea na hivyo kufanya nchi wanachama wa benki hiyo kufika 86.

Kenya inatazmiwa kunufaika na benki hiyo muhimu ya bara Asia na hivyo kupunguza utegemezi wake kwa benki za nchi za Magharibi. Hatua ya Kenya kujiunga na benki hiyo ambayo makao yake makuu yako mjini Beijing inatathminiwa kuwa hatua nyingine ya nchi hiyo kujikurubisha kwa China, nchi ambayo kwa sasa imekuwa ikifadhili miradi ya miundo mbinu katika nchi hiyo.

Barabara mpya ya Hariri iliypendekezwa na China

Wachambuzi nchini Kenya wamepongeza hatua ya serikali ya Kenya kujiunga na benki hiyo. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kenyatta Ken Ogembo ameliambia Shirika la Habari la Xinhua kuwa, kwa miaka mingi Kenya imekuwa nyuma kwenye maendeleo ya miundo mbinu, kutokana na masharti ya mikopo yanayowekwa na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa.

China hivi sasa iko katika mkakati wa kuimarisha miundo msingi hasa ya usafiri katika maeneo ya Asia, Ulaya na Afrika ili kufikia lengo lake la kuhuisha ukanda wa kale wa usafiri unaojulikana kama Barabara ya Hariri.