Rais Kenyatta asaini sheria kali kwa wahalifu mitandaoni
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i44566-rais_kenyatta_asaini_sheria_kali_kwa_wahalifu_mitandaoni
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameidhinisha Sheria za Uhalifu wa Kompyuta na Mtandaoni wa 2018 ambazo zinatoa adhabu kali sana kwa watakaopatikana na makosa ya mtandaoni ikiwa ni pamoja na kueneza habari bandia au feki.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 16, 2018 13:59 UTC
  • Rais Kenyatta asaini sheria kali kwa wahalifu mitandaoni

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameidhinisha Sheria za Uhalifu wa Kompyuta na Mtandaoni wa 2018 ambazo zinatoa adhabu kali sana kwa watakaopatikana na makosa ya mtandaoni ikiwa ni pamoja na kueneza habari bandia au feki.

Kwa mujibu wa sheria hiyo atakayepatikana na kosa la uenezaji wa habari za uzushi na bandia, atakabiliwa na adhabu  ya faini ya Sh5 milioni (takribani dola 50,000 za Marekani) au kifungo cha miaka miwili jela, au adhabu zote mbili, kwa

Mtu atakayepatikana na kosa la kueneza taarifa ambazo zinaweza kuzua taharuki au kuzua vurugu atafungwa jela zaidi ya miaka kumi.

Halikadhalika sheria hiyo pia inalenga kuchukua hatua kali za kuwaadhibu wadukuzi wa kompyuta au hackers ambapo atakayepatikana na kosa hilo atatozwa faini ya shilingi milioni tano au kufungwa jela miaka mitatu  au yote mawili kwa kosa la kuingia bila idhini katika mitandao ya intaneti ya wengine au kufanya ujasusi wa kiintaneti.

Sheria hiyo inatarajiwa kuathiri utendakazi wa wanahabari, vyombo vya habari, watumiaji wa mitandao ya kijamii, wanablogu na watu wengine wanaotumia kompyuta na mitandao. Halikadhalika sheria hiyo pia inatoa adhabu kali kwa wanaoeneza picha za ngono za watoto.

Kiongozi wa zamani wa Chama cha Wanasheria Kenya Apollo Mboya amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kifungu hicho kinaweza kuwapa watawala 'uhuru' wa kukandamiza vyombo vya habari.