Wananchi wa Morocco waandamana kulaani kuhamishiwa Quds ubalozi wa Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i44780-wananchi_wa_morocco_waandamana_kulaani_kuhamishiwa_quds_ubalozi_wa_marekani
Makumi ya maelfu ya wananchi wa Morocco wamefanya maandamano katika mji wa Dār al-Bayḍā (Casablanca) kulaani hatua ya Marekani ya kuuhamishia Quds ubalozi wake uliokuweko Tel Aviv, mji mkuu wa utawala pandikizi wa Israel.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 21, 2018 07:57 UTC
  • Wananchi wa Morocco waandamana kulaani kuhamishiwa Quds ubalozi wa Marekani

Makumi ya maelfu ya wananchi wa Morocco wamefanya maandamano katika mji wa Dār al-Bayḍā (Casablanca) kulaani hatua ya Marekani ya kuuhamishia Quds ubalozi wake uliokuweko Tel Aviv, mji mkuu wa utawala pandikizi wa Israel.

Shirika la habari la IRIB limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, katika maandamano hayo, wananchi wa Morocco wamebeba bendera za Palestina na kutoa nara za "Mauti kwa Israel." Waandamanaji hao wamebeba mabango yaliyokuwa na maandishi yasemayo: "Quds ni mji mkuu wa milele wa Palestina."

Tarehe 6 Disemba 2017, rais wa Marekani, Donald Trump alidharau kelele zote za kimataifa na alitangaza kuwa anaitambua Quds yenye Kibla cha Kwanza cha Waislamu kuwa eti ni mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Jumatatu iliyopita, Trump alitekeleza msimamo wake huo kupitia kuuhamishia Quds ubalozi wa Marekani uliokuweko Tel Aviv.

Sehemu ya maandamano ya wananchi wa Morocco ya kupinga uamuzi wa Trump kuhamishia Quds ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv

 

Tangu wakati huo hadi hivi sasa maandamano yanafanyika katika kona mbalimbali za dunia hasa huko Palestina kulaani uadui huo wa Donald Trump kwa ulimwengu wa Kiislamu.

Wanajeshi katili wa Israel wameungana na Trump kufanya jinai dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Palestina kwa kukandamiza kinyama maandamano ya Wapalestina hao na kuua kwa umati watu 65 na kujeruhi wengine zaidi ya 2900.

Mji mtakatifu wa Baytul Muqaddas ambao una Kibla cha Kwanza cha Waislamu ni mji mkuu wa milele wa Palestina na ni moja ya maeneo matatu matukufu zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu. Mji huo unakaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel tangu mwaka 1967.