Jun 22, 2018 07:50 UTC
  • Waasi Sudan Kusini: Muda zaidi unahitajika kufikia amani

Waasi wa Sudan Kusini wametangaza kuwa muda zaidi unahitajika ili kufanikisha mchakato wa amani ya kudumu nchini humo na kwamba itakuwa jambo la muhimu kuvipatia ufumbuzi vyanzo vikuu vya vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Sudan Kusini.

Waasi nchini Sudan Kusini wamesema katika taarifa yao baada ya mazungumzo ya amani yaliyofanyika Ethiopia kati ya kiongozi wa kundi hilo la waasi Riek Machar na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini. Hiyo ilikuwa mara ya kwanza viongozi hao kukutana tangu mwaka 2016 baada ya makubaliano ya amani kuvunjika na kuibuka tena mapigano kati ya vikosi vya pande mbili hizo.

Riek Machar kiongozi wa waasi Sudan Kusini (kulia)akiwa Addis Ababa kwa mazungumzo na Rais Salva Kiir
 

Waasi wa Sudan wa SPML/SPLA (IO) wamesema kuwa ufumbuzi wa vita vya ndani vya miaka mitano nchini humo vilivyouwa makumi ya maelfu ya watu na kuwalazimisha wengine zaidi ya milioni tatu kuwa wakimbizi ni kuurejelea mkataba mkuu wa amani ujulikanao kama (CPA).

Mkataba huo wa amani ulifikiwa mwaka 2005 kati ya Sudan na Sudan Kusini kwa lengo la kuhitimisha vita vya ndani huko Sudan na kuifungulia njia Sudan Kusini kuweza kujitenga.

Tags