Vikao vya Bunge la Afrika vyaanza mjini Kigali Rwanda + Sauti
(last modified Mon, 22 Oct 2018 17:02:13 GMT )
Oct 22, 2018 17:02 UTC

Bunge la Afrika limefungua kikao chake cha wiki mbili mjini Kigali Rwanda ambapo kwa muda wa wiki mbili wabunge wake watajadili mambo kadhaa kuhusu demokrasia,uongozi bora na kurahisisha mafungamano ya biashara baina ya waafrika wenyewe. Ni kikao kilichofunguliwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.