Mahakama ya Katiba Madagascar yathibitisha ushindi wa Andry Rajoelina
(last modified Wed, 09 Jan 2019 04:41:38 GMT )
Jan 09, 2019 04:41 UTC
  • Mahakama ya Katiba Madagascar yathibitisha ushindi wa Andry Rajoelina

Mahakama ya Katiba ya Madagascar imethibitisha ushindi wa Andry Rajoelina na kutupilia mbali madai ya kuweko udanganyifu yaliyowasilisha na hasimu wake Marc Ravalomanana.

Mkuu wa Mahakama ya Katiba ya Madagascar Eric Rakotoarisoa  ametangaza kuwa, mahakama hiyo inathibitisha kwamba, Andry Rajoelina ndiye mshindi wa kiti cha urais katika uchaguzi wa duru ya pili baada ya kupata asilimia 55.66 ya kura. 

Akthari ya wagombea wa kiti cha urais nchini Madagascar walikuwa wametangaza kuwa, hawangepinga matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi huo uliofanyika tarehe 19 Disemba. Hata hivyo siku chache baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa duru ya pili, timu ya kampeni ya Marc Ravalomanana iliwasilisha mashtaka katika Mahakama ya Katiba ya nchi hiyo ikitaka kufutwa matokeo ya uchaguzi huo ikidai kwamba, kulifanyika udanganyifu.

Marc Ravalomanana

Katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais iliyofanyika tarehe 19 Disemba, 2018, Ravalomama alishindwa kwa kupata asilimia 44 ya kura mbele ya mpinzani wake Andry Rajoelina aliyepata asimilia 55 ya kura hizo kwa mujibu wa matokeo rasmi.

Timu ya Ravalomanana iliwasilisha mashtaka katika Mahakkama ya Katiba kupinga matokeo ya uchaguuzi katika hali ambayo, wasimamizi wa uchaguzi walitangaza kwamba, duru ya pili ya uchaguzi huo ilifanyika kisheria na hakukuwa na aina yoyote ile ya udanganyifu.

Mahasimu hao wawili wa kisiasa Marc Ravalomanana na Andry Rajoelina waliwahi kuwa marais wa Madagascar kabla ya uchaguzi wa mwaka jana.