Rais mteule wa Afrika Kusini kuapishwa Mei 25, Siku ya Afrika
Ofisi ya Rais nchini Afrika Kusini imetangaza kuwa sherehe za kuapishwa kwa rais mteule zitafanyika Mei 25 ambayo huadhimsihwa duniani kote kama Siku ya Afrika.
Kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya rais Khusela Diko kufanyika kwa sherehe hizo katika Siku ya Afrika ni ishara muhimu, kwani inathibitisha nia ya serikali ya kuboresha ajenda ya Afrika na kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika Kusini na majirani zake.
Kauli mbiu ya sherehe za kuapishwa ni "Kwa Pamoja Tunasherehekea Miaka 25 ya Uhuru: Kurejesha Tena na Ukuaji kwa ajili ya Afrika Kusini iliyo Bora."
Sherehe hizo zinatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa nchi mbali mbali , pamoja na wawakilishi wa dini, vyama vya siasa na jumuiya za kieneo na kimataifa.Uchaguzi mkuu Afrika Kusini umepengwa kufanyika Mei 8 kuchagua Bunge la Kitaifa na pia mabunge ya mikoa. Uchaguzi huu utakuwa ni wa sita tangu kupinduliwa mfumo wa utawala wa ubaguzi wa rangi mwaka 1994. Uchaguzi huu pia unatazamiwa kuainsha rais ajaye wa nchi hiyo.
Rais wa sasa Cyril Ramaphosa ataongoza chama tawala cha ANC ambacho kinaleng akuendelea kuwa na viti vingi bungeni. Ramaphosa alichukua urais Februari 2018 baada ya aliyemtangulia kujiuzulu kufuatia tuhuma za ufisadi.