Arab League yaunga mkono mapatano yaliyofikiwa kati ya makundi ya Sudan
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i54617-arab_league_yaunga_mkono_mapatano_yaliyofikiwa_kati_ya_makundi_ya_sudan
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) ameunga mkono mapatano yaliyofikiwa kati ya Baraza Kuu la Kijeshi la Uongozi wa Mpito Sudan na makundi ya upinzani kwa ajili ya kuunda baraza la uongozi la kipindi cha mpito.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 07, 2019 22:11 UTC
  • Arab League yaunga mkono mapatano yaliyofikiwa kati ya makundi ya Sudan

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) ameunga mkono mapatano yaliyofikiwa kati ya Baraza Kuu la Kijeshi la Uongozi wa Mpito Sudan na makundi ya upinzani kwa ajili ya kuunda baraza la uongozi la kipindi cha mpito.

Akiwa ziarani katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, Khalil Ibrahim al Thawadi amebainisha kufurahishwa Jumuiya ya Arab League na mapatano hayo kati ya Baraza la Kijeshi la Uongozi wa Mpito na Muungano wa Uhuru na Mabadiliko kuhusu kuunda baraza la uongozi nchini humo. Khalil al Dhawadi amesema kuwa mapatano hayo yameungwa mkono na makundi yote ya kisiasa na pande zote zinataka kuweko umoja na mshikamano na kufanyika jitihada ili kuondokana na taathira za zama zilizopita. 

Baraza la kijeshi la Sudan

Pande mbili za Baraza la Kijeshi la Uongozi wa Mpito la Sudan na muungano wa upinzani kwa jina la Uhuru na Mabadiliko Alhamisi iliyopita zilifikia mapatano ya kuunda serikali ya kiraia na baraza la uongozi kwa muda wa miaka mitatu ambalo rais wake atakuwa wa kiduru. Mapatano hayo yalifikiwa na pande mbili hizo baada ya kufanyika mazungumzo ya moja kwa moja. Baraza la Kijeshi la Uongozi wa Mpito la Sudan lilishika hatamu za uongozi baada ya mapinduzi ya tarehe 11 Aprili mwaka huu yaliyomuengua madarakani Rais Omar al Bashir wa nchi hiyo.