Wanachama 10 wa Boko Haram wauawa Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i5650-wanachama_10_wa_boko_haram_wauawa_nigeria
Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa limeua wanachama 10 wa kundi la kigaidi la Boko Haram katika operesheni iliyofanyika kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 23, 2016 08:10 UTC
  • Wanachama 10 wa Boko Haram wauawa Nigeria

Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa limeua wanachama 10 wa kundi la kigaidi la Boko Haram katika operesheni iliyofanyika kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Msemaji wa jeshi la Nigeria, Sani Usman amesema kuwa, wapiganaji hao wa Boko Haram wameuawa katika operesheni ya jeshi ya kusafisha maeneo ya kaskazini mwa jimbo la Borno. Sani Usman ameongeza kuwa, katika operesheni hiyo jeshi la Nigeria limewakomboa mateka 7 waliokuwa wakishikiliwa na kundi hilo la kigaidi na kuwatia nguvuni wapiganaji kadhaa na silaha zao.

Kundi la Boko Haram lililoanzisha machafuko ya ndani nchini Nigeria mwaka 2009 limeua zaidi ya watu elfu 20 na kulazimisha mamilioni ya wengine kukimbia maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo. Kundi hilo pia limepanua mashambulizi yake ya kigaidi katika nchi jirani kama Cameroon, Chad na Niger.