Leo ni siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani nchini Iran
(last modified Sat, 25 Apr 2020 04:07:00 GMT )
Apr 25, 2020 04:07 UTC
  • Leo ni siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani nchini Iran

Leo Jumamosi ni siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Ofisi ya Kusambaza Athari za Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiisalmu imetangaza kuwa, kamati za kutafuta mwezi zilitumwa kote Iran siku ya Alhamisi na kwa kutumia vifaa vya kitaalamu mwezi haukuweza kuonekana.

Kwa msingi huo leo Jumamosi imetangazwa kuwa siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika mwaka 1441 Hijria Qamaria.

  Sheikh Ahmad Muhdhar Kadhi Mkuu wa Kenya ametangaza kuwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani nchini humo utaanza Aprili 25 2020

Ofisi ya Ayatullah Sistani, marjaa mkuu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq naye pia ametangza kuwa leo Jumamosi ni siku ya kwanza ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Baadhi ya nchi za Kiarabu kama vile  Syria, Imarati, Saudi Arabia na Kuwait zilianza mwezi Mtukufu wa Ramadhai jana Ijumaa. Aidha nchi zingine za Kiarabu kama vile Oman, Morocco na pia nchi za Afrika Mashariki zinaanza rasmi Saumu ya Ramadhani leo Jumamosi.