Wajumbe wa Baraza la Usalama la UN kutembelea Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i6289-wajumbe_wa_baraza_la_usalama_la_un_kutembelea_somalia
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanatazamiwa kutembelea Somalia katika siku chache zijazo ili kuonyesha uungaji mkono kwa uchaguzi ujao nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 03, 2016 02:30 UTC
  • Wajumbe wa Baraza la Usalama la UN kutembelea Somalia

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanatazamiwa kutembelea Somalia katika siku chache zijazo ili kuonyesha uungaji mkono kwa uchaguzi ujao nchini humo.

Kwa mujibu wa Amr Aboulatta, balozi wa Misri katika Umoja wa Mataifa na mwenyekiti wa kiduru wa Baraza la Usalama, ujumbe wa baraza hilo utafika pia Nairobi mji mkuu wa Kenya na makao makuu ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu mjini Misri katika safari hiyo itakayoanza Mwezi 17-21.

Ameongeza kuwa, uchaguzi mkuu nchini Somalia utafanyika mwezi Agosti mwaka huu na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaunga mkono kufanyika uchaguzi huo.

Uchaguzi huo utakuwa wa pili tangu vita vya ndani vianze Somalia mwaka 1991.

Uchaguzi mwingine ulifanyika mwaka 2012.

Baraza la mawaziri na viongozi wa kitaifa wa Somalia katika kikao chao tarehe 28 Januari mjini Mogadishu waliafiki kuwa baraza la mawaziri litavunjwa kabla ya uchaguzi ili kuandaa mazingira ya kufanyika uchaguzi wa rais na wa bunge.