Iran na Nigeria kushirikiana zaidi katika masuala ya nishati
(last modified Thu, 24 Sep 2020 02:43:40 GMT )
Sep 24, 2020 02:43 UTC
  • Iran na Nigeria kushirikiana zaidi katika masuala ya nishati

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Nigeria zimetilia mkazo wajibu wa kustawishwa uhusiano wao katika nyuga mbalimbali hasa za nishati kwa kadiri inavyowezekana.

Hayo yamebainishwa katika mazungumzo yaliyofanyika baina ya Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu na Waziri wa Mafuta wa Nigeria mjini Abuja ambapo pande hizo mbili zimesema zina uwanda mpana wa kustawisha uhusiano wao hasa katika sekta ya nishati.

Shirika la habari la IRNA limetangaza habari hiyo na kumnukuu Mohammad Ali Bak, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akisema katika mazungumzo yake hayo na Timipara Silva, Waziri wa Mafuta wa Nigeria kwamba, kwa vile Nigeria ni mwanachama wa OPEC na hivi sasa Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo ya wazalishaji wakubwa wa mafuta duniani ni raia wa Nigeria na vile vile kutokana na Nigeria kuwa mwanachama wa OPEC ya gesi, yote hayo yameandaa nyuga nyingi za ushirikiano wa pamoja baina ya Tehran na Abuja na kuna udharura wa pande hizi mbili kushirikiana kwa upana mkubwa zaidi katika masuala ya gesi na mafuta.

Bendera za Iran na Nigeria

 

Katika mazungumzo hayo, pande hizo mbili zimesisitizia pia udharura wa kutumiwa vizuri fursa zote zinazojitokeza za kustawisha uhusiano wa nchi hizi mbili zikiwemo hizo za kuwa wanachama wa jumuiya mbili za OPEC ya mafuta na OPEC ya gesi ambayo inajulikana kwa jina la Jukwaa la Nchi Zinazosafirisha Nje Gesi kwa Wingi (GECF).