Waziri Mkuu wa Ethiopia: Jeshi limefanikiwa dhidi ya harakati ya TPLF
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i64438-waziri_mkuu_wa_ethiopia_jeshi_limefanikiwa_dhidi_ya_harakati_ya_tplf
Abiy Ahmed Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema kuwa mashambulizi ya Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Tigray (The Tigray People's Liberation Front (TPLF)) yamedhibitiwa. Amesema jeshi la Ethiopia litatekeleza oparesheni nyingine siku chache zijazo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 05, 2020 04:31 UTC
  • Waziri Mkuu wa Ethiopia: Jeshi limefanikiwa dhidi ya harakati ya TPLF

Abiy Ahmed Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema kuwa mashambulizi ya Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Tigray (The Tigray People's Liberation Front (TPLF)) yamedhibitiwa. Amesema jeshi la Ethiopia litatekeleza oparesheni nyingine siku chache zijazo.

Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema kuwa jeshi limefanikiwa kuzima uasi wa harakati ya TPLF huko kaskazini mwa Tigray baada ya kutumwa huko kuzima uasi uliokuwa umeanzishwa na harakati hiyo; jambo lililoibua wasiwas wa kuibuka vita vya ndani. Serikali ya Addis Ababa aidha imeliweka eneo la Tigray katika hali ya hatari kwa muda wa miezi sita. Eneo hilo linapakana na Eritrea.  

Abiy Ahmed ambaye ni mshindi wa tuzo ya Nobel jana jioni alihutubia taifa kwa njia ya televisheni na kusema: Jeshi la nchi hiyo si tu kuwa limefanikiwa kurudisha nyuma mashambulizi ya harakati ya TPLF bali limeweza kudhibiti maeneo muhimu. Waziri Mkuu wa  Ethiopia hata hivyo hakutaja ni watu wangapi wameuliwa kwenye oparesheni hiyo ya jeshi. Jeshi la Ethiopia kwa upande wake limetangaza kuwa limeisababishia maafa makubwa Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Tigray.

Wapiganaji wa harakati ya Tigray ya TPLF 

Itakumbukuwa kuwa mashambulizi hayo ya jeshi la Ethiopia yametekelezwa kwa amri ya Waziri Mkuu wa Ethiopia.

Mapema jana Abiy Ahmed alieleza kuwa harakati hiyo juzi ilifanya jaribio la kudhibiti kambi ya jeshi ya kaskazini mwa nchi hiyo kwa nia ya kutwaa silaha zilizoko kwenye kambi hiyo.

Alisema harakati ya TPLF imechagua vita; na hivyo jeshi limelazimika kuchukua hatua.