Waziri Mkuu wa Ethiopia awapatia siku tatu waasi wa Tigray wajisalimishe
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i64623-waziri_mkuu_wa_ethiopia_awapatia_siku_tatu_waasi_wa_tigray_wajisalimishe
Waziri Mkuu wa Ethiopia amewapatia waasi wa Tigray wanaojulikana kama Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Tigray (The Tigray People's Liberation Front (TPLF) kaskazini mwa nchi hiyo muda wa siku tatu kuanzia jana wasitishe uasi wao na kujisalimisha.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 14, 2020 08:42 UTC
  • Waziri Mkuu wa Ethiopia awapatia siku tatu waasi wa Tigray wajisalimishe

Waziri Mkuu wa Ethiopia amewapatia waasi wa Tigray wanaojulikana kama Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Tigray (The Tigray People's Liberation Front (TPLF) kaskazini mwa nchi hiyo muda wa siku tatu kuanzia jana wasitishe uasi wao na kujisalimisha.

Abiy Ahmed amesema hayo katika hotuba yake kwa njia ya televisheni na kueleza kwamba, Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Tigray imezingirwa katika maeneo na ngome zake zote na haiwezi tena kutoa maagizo kwa wapiganaji wake.

Waziri Mkuu wa Ethiopia ameisitiza kuwa, waasi hao wana muda wa siku tatu kuanzia jana Ijumaa wajisalimishe

Aidha amewataka wazi katika jimbo la Tigray kutowatuma watoto wao katika vita na vikosi vya serikali.

Wakati hu huo, jana Jeshi la Ethiopia lilitangaza kuwa limefanya mashambulio katika maghala ya silaha na kambi za kuhifadhia nishati za Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Tigray (The Tigray People's Liberation Front (TPLF)) kaskazini mwa nchi hiyo.

Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa Ethiopia

 

Ripoti zinasema kuwa, mamia ya wapiganaji kutoka pande mbili wameuliwa na kujeruhiwa katika mapigano baina ya jeshi la Ethiopia na wanamgambo wa Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Tigray.

Tigray ni eneo la jamii ya wachache lakini wenye nguvu ambao kwa miongo kadhaa wamekuwa wakiongoza muungano tawala nchini Ethiopia.  

Muungano mpya wa utawala ulioundwa miaka miwili iliyopita baada ya kuingia madarakani Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed umesusiwa na jamii ya watu wa Tigray.

Mzozo huo wa serikali ya Ethiopia na jimbo lake la kaskazini la Tigray umevuka mpaka baada ya maelfu ya watu kuhamia nchini Sudan, pamoja na wanajeshi walioasi.