May 08, 2016 07:35 UTC
  • Nkosazana Dlamini Zuma, Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika AU
    Nkosazana Dlamini Zuma, Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika AU

Umoja wa Afrika AU umeelezea kusikitishwa sana na kiwango cha juu cha ufisadi katika nchi za bara hilo.

Bi Nkosazana Dlamini Zuma, Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika alisema jana jijini Nairobi Kenya kuwa, ufisadi unawafanya wananchi kukosa imani na serikali za nchi za Afrika.

Dlamini Zuma ameongeza kuwa, wananchi wanapenda kuiga mtindo wa maisha ya watu ambao matumizi yao ni makubwa na hayaendani na kipato chao na hiyo ndiyo sababu kuu ya kuenea ufisadi barani Afrika.

Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika ameongeza kuwa, kuna baadhi ya nchi za Afrika zimeanza kutekeleza kivitendo sheria za kupambana na ufisadi.

Amesema, ufisadi unashadidisha umaskini katika bara la Afrika licha ya bara hilo kuwa na utajiri mkubwa wa maliasili.

Tags