Sep 30, 2021 06:28 UTC
  • Sheikh Zakzaky: Matembezi ya Arubaini ya Imam Husain AS yataendelea Nigeria

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesisitiza kuwa, matembezi ya Arubaini ya Imam Husain AS yataendelea kufanyika nchini Nigeria hadi atakapodhihiri Imam wa Zama, Imam Mahdi AS.

Sheikh Ibrahim Zakzaki alisema hayo jana usiku katika mahojiano maalumu aliyofanyiwa na televisheni ya Press TV na kuongeza kuwa, matembezi ya Arubaini ya Imam Husain AS yataendeleaa hadi atakapodhihiri Imam Mahdi AS na askari wa serikali ya Nigeria hawawezi kukwamisha matembezi hayo kwa kuwapiga kwao risasi Waislamu wanaoshiriki kwenye matembezi hayo. 

Mahojiano hayo yamefanyika katika hali ambayo jeshi la polisi la Nigeria siku ya Jumanne liliwashambulia Waislamu waliokuwa wanashiriki katika matembezi ya Arubaini ya Imam Husain AS na kuwaua shahidi Waislamu wanane.

Abdullah Muhammad, mwanachama mwandamizi wa harakati hiyo amesema, walioshiriki kwenye matembezi ya Arubaini ya Imam Husain AS walikuwa wanafanya matembezi hayo kwa njia ya amani bila ya kuhatarisha usalama wa mtu yeyote, lakini pamoja na hayo polisi waliwafyatulia risasi Waislamu hao na kuwaua shahidi wanane kati yao.

Sheikh Ibrahim Zakzaky

 

Tags