Kodivaa yamkamata mshukiwa wa ulipuaji bomu hoteli ya Grand Bassam
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i7909-kodivaa_yamkamata_mshukiwa_wa_ulipuaji_bomu_hoteli_ya_grand_bassam
Wakuu wa Kodivaa wamesema wamemkamata mtu anayeshukiwa kusafirisha silaha zilizotumika katika hujuma ya kigaidi ilyopelekea watu 19 kuuawa katika hoteli moja ya kifahari ya Grand Bassam nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 27, 2016 03:24 UTC
  • Kodivaa yamkamata mshukiwa wa ulipuaji bomu hoteli ya Grand Bassam

Wakuu wa Kodivaa wamesema wamemkamata mtu anayeshukiwa kusafirisha silaha zilizotumika katika hujuma ya kigaidi ilyopelekea watu 19 kuuawa katika hoteli moja ya kifahari ya Grand Bassam nchini humo.

Televisheni ya Kitaifa ya Kodivaa imetangaa kuwa, dereva aliyesafirisha silaha zilitotumiwa na magaidi waliotekeleza hujume hiyo katika ufukwe wa bahari alikamatwa Alhamisi na kwamba hivi sasa anasailiwa.

Taarifa zinasema aliyekamatwa ametambuliwa kama Barry Battesi mwenye umri wa miaka 24 na kwamba alikuwa mafichoni kusini mwa mji wa Abidjan.

Ikumbukwe kuwa Mnamo Machi 13 magaidi waliwashambulia watalii na wananchi waliokuwa katika hoteli ya kifahari ya Grand Bassam katika mji mkuu wa kibiashara wa Kodivaa, Abidjan na kuwaua watu 19. Kundi la kigaidi la Al Qaeda lilidai kuhusika na hujuma hiyo. Tayari watu 17 wameshakamatwa kuhusiana na shambulio hilo ingawa kinara wao, Kounta Dallah bado hajakamatwa.