Mawaziri wawili wa serikali mpya ya Libya watekwa nyara
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i81000-mawaziri_wawili_wa_serikali_mpya_ya_libya_watekwa_nyara
Kundi la wanamgambo wenye silaha limewateka nyara mawaziri wawili wa serikali mpya ya nchi hiyo.
(last modified 2025-11-07T02:31:33+00:00 )
Mar 04, 2022 08:04 UTC
  • Mawaziri wawili wa serikali mpya ya Libya watekwa nyara

Kundi la wanamgambo wenye silaha limewateka nyara mawaziri wawili wa serikali mpya ya nchi hiyo.

Vyombo vya habari vya Libya vimeripoti kuwa, kundi la watu waliokuwa na silaha lenye mfungamano na aliyekuwa waziri mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya, Abdul Hamid Dbeibah limewatia nguvuni Waziri wa Utamaduni na Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali mpya ya Libya inayoongozwa na Waziri Mkuu, Fat'hi Bashagha.

Jumatano iliyopita Fat'hi Bashagha alisema kwamba Abdul Hamid Dbeibah amefunga anga ya Libya ili kuzuia mawaziri wapya kuelekea Tobruk kwa ajili ya kula kiapo.

Katika hotuba yake iliyotangazwa na vyombo vya habari vya Libya, Abdul Hamid Dbeibah amelishutumu Bunge la nchi hiyo kwa kuiba kura, akisema kura ya kuwa na imani na Bashagha haikutimiza akidi.

Abdul Hamid Dbeibah

Vyombo vya habari vya Libya tarehe 10 Februari viliripoti kwamba Fat'hi Bashagha amechaguliwa kwa wingi mkubwa wa kura za Bunge la Libya kuwa Waziri Mkuu mpya na mrithi wa Abdul Hamid Dbeibah.