Mkuu wa intelijenisia wa kundi la al Shabaab auawa Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i8278-mkuu_wa_intelijenisia_wa_kundi_la_al_shabaab_auawa_somalia
Vikosi vya usalama vya Somalia vimemuuwa mkuu wa kitengo cha intelijinsia cha kundi la wanamgambo wa al Shabaab. Hayo yamesemwa leo na afisa wa serikali ya Somalia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 01, 2016 11:29 UTC
  • Mkuu wa intelijenisia wa kundi la al Shabaab auawa Somalia

Vikosi vya usalama vya Somalia vimemuuwa mkuu wa kitengo cha intelijinsia cha kundi la wanamgambo wa al Shabaab. Hayo yamesemwa leo na afisa wa serikali ya Somalia.

Abdifatah Omar msemaji wa manispaa ya Mogadishu amesema kuwa majasusi wamemuuwa mkuu huyo wa intelijinsia wa kundi la al Shabaab anayejulikana kwa jina la Daud ambaye alikuwa akiliongoza tawi la kiitelijinsia la kundi hilo ambalo linajulikana kwa jina la "Amniyat".

Hadi kufikia sasa al Shabaab haijatoa taarifa yoyote kuhusu mauaji hayo. Kundi la wanamgambo wa al Shabaab ambalo limedhamiria kuing'oa madarakani serikali ya Somalia lilifurushwa katika mji mkuu Mogadishu na askari jeshi wa kulinda Amani walioko Somalia AMISOM mwaka 2011, na mwaka jana kundi hilo lilifurushwa katika ngome zake za kusini mwa Somalia na wanajeshi hao wa kulinda amani kwa kushirikiana na jeshi la serikali ya Somalia.