Apr 28, 2022 02:45 UTC
  • Mashabiki wa mpira wapiga nara za

Nara ya "Palestina! Palestina!" imerindima katika uwanja wa mpira wa miguu kutoka kwa mashabiki wa mchezo huo nchini Morocco, nchi ambayo imetangaza uhusiano wa kawaida na Wazayuni kinyume na msimamo wa wananchi wa nchi hiyo.

Kanali ya Telegram ya "Ghaza al Aan" imesambaza mkanda wa video unaoonesha mashabiki wa kandanda nchini Morocco wakipiga nara za "Palestina! Palestina!" ili kutangaza uungaji mkono wao kwa taifa linalodhulumiwa la Palestina.

Wananchi wa Morocco wana historia ya kuliunga mkono taifa madhlumu la Palestina licha ya viongozi wa nchi hiyo kujipendekeza kwa Wazayuni kupitia kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala dhalimu wa Israel.

Msikiti wa al Aqsa, Kibla cha Kwanza cha Waislamu

 

Licha ya makubalino ya nchi za Kiarabu ya kuheshimu kikamilifu malengo matukufu ya ukombozi wa Palestina, lakini nchi za Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati), Bahrain, Sudan na Morocco ziliamua kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni katika kipindi cha baina ya miezi ya Septemba hadi Disemba 2020.

Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Morocco pamoja na wanasiasa wa nchi hiyo, hadi leo wanaendelea kupinga hatua ya serikali ya Rabbat ya kujidhalilisha mbele ya Wazayuni na kutangaza kwake uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel licha ya jambo hilo kuwa ni usaliti mkubwa kwa kadhia ya Palestina.

Tags