Wapinzani wa serikali ya DRC wakutana nchini Ubelgiji
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i8872-wapinzani_wa_serikali_ya_drc_wakutana_nchini_ubelgiji
Vyombo vya habari vimeripoti habari ya kukutana wapinzani wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini Ubelgiji.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 10, 2016 02:52 UTC
  • Wapinzani wa serikali ya DRC wakutana nchini Ubelgiji

Vyombo vya habari vimeripoti habari ya kukutana wapinzani wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini Ubelgiji.

Habari zinasema kuwa, wapinzani hao wamekutana mapema leo Ijumaa karibu na Brussels, mji mkuu wa Ubelgiji wakimtaka Rais Joseph Kabila wa DRC ang'oke madarakani.

Etienne Tshisekedi, mkuu wa chama cha upinzani cha UDPS na ambaye alishiriki katika uchaguzi wa Rais nchini Kongo mwaka 2011 na kushindwa, amesema mbele ya takriban wawakilishi mia moja wa jumuiya za kijamii na wapinzani wa serikali ya Kongo kwamba, ana uhakika wapinzaniwatashinda kwa hali yoyote.

Makubaliano baina ya vyama vya upinzani vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamefikiwa baada ya kufanyika kikao cha siku mbili cha faragha.

Kikao hicho kiliitishwa na mkuu wa chama cha UDPS, Etienne Tshisekedi na wapinzani wamekubaliana kuunganisha nguvu zao kwa ajili ya kuhakikisha Rais Joseph Kabila anang'oka madarakani huko Kongo.

Muungano huo mpya umeunda kamati inayoongozwa na Tshisekedi kwa ajili ya kusimamia hatua zitakazochukuliwa na wapinzani katika kampeni zao hizo.