Jeshi Nigeria laangamiza Boko Haram
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i9184-jeshi_nigeria_laangamiza_boko_haram
Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa, limefanikiwa kusafisha maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo kwa kuangamiza makumi ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la Boko Haram.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 14, 2016 12:46 UTC
  • Jeshi Nigeria laangamiza Boko Haram

Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa, limefanikiwa kusafisha maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo kwa kuangamiza makumi ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la Boko Haram.

Msemaji wa jeshi la Nigeria, Kanali Sani Othman, amesema kuwa jeshi hilo limefanikiwa kugundua maficho mengine ya genge la Boko Haram huko kaskazini mwa Nigeria na kuangamiza makumi ya wapiganaji wa kundi hilo. Kanali Othman amongeza kuwa, katika mashambulizi mengine yaliyofanyika jana jeshi la Nigeria liliharibu maficho kadhaa ya magaidi wa Boko Haram katika vijiji 13 vya eneo la Bama.

Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema kuwa katika operesheni hiyo iliyofanyika kwenye jimbo la Borno mateka 225 waliokuwa wakishikiliwa na magaidi wamekombolewa.

Maelfu ya watu wameuawa tangu kundi la kigaidi la Boko Haram lianze mashambulizi yake nchini Nigeria na katika nchi kadhaa jirani hapo mwaka 2009.