Mafuriko yaua watu 10 kusini mwa Uganda, mamia walazimishwa kuhama makazi yao
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i92198-mafuriko_yaua_watu_10_kusini_mwa_uganda_mamia_walazimishwa_kuhama_makazi_yao
Maafisa wa serikali ya Uganda wametangaza kuwa mafuriko yaliyotokea jana kusini mwa nchi hiyo yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 10.
(last modified 2025-11-07T02:31:33+00:00 )
Dec 28, 2022 04:21 UTC
  • Mafuriko yaua watu 10 kusini mwa Uganda, mamia walazimishwa kuhama makazi yao

Maafisa wa serikali ya Uganda wametangaza kuwa mafuriko yaliyotokea jana kusini mwa nchi hiyo yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 10.

Ripoti zinasema kuwa, zaidi ya familia 400 zimelazimishwa kuhama makazi yao katika wilaya za Rakai na Lyantonde. 

Mvua kubwa iliyonyesha Desemba 20 imepelekea kujaa maji Mto Rwizi na Ziwa Kijjanibarora na kusababisha mafuriko katika vijiji kadhaa jirani.

Waziri wa Habari wa eneo la Kooki, Stanley Ndawula, amesema Daraja la Kibaale, ambalo linaunganisha eneo hilo na barabara kuu inayoelekea mji mkuu, Kampala, pia liko hatarini kutokana na mafuriko hayo.

William Oketa, afisa wa polisi katika eneo hilo amesema vifo vya watu 10 vimethibitishwa kufikia sasa, na ametoa wito kwa watu wanaoishi katika maeneo ya karibu kuhamia kwenye maeneo salama.