Nigeria, Chad, Niger zaanzisha oparesheni ya pamoja dhidi ya Boko Haram
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i9721-nigeria_chad_niger_zaanzisha_oparesheni_ya_pamoja_dhidi_ya_boko_haram
Majeshi ya Nigeria, Niger na Chad yameanzisha oparesheni ya pamoja dhidi ya magaidi wakufurishaji wa Boko Haram.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 22, 2016 07:07 UTC
  • Nigeria, Chad, Niger  zaanzisha oparesheni ya pamoja dhidi ya Boko Haram

Majeshi ya Nigeria, Niger na Chad yameanzisha oparesheni ya pamoja dhidi ya magaidi wakufurishaji wa Boko Haram.

Kwa mujibu wa Brigedia Jenerali Abdou Sidikou Issa, kamanda wa jeshi la Niger katika eneo la Diffa amesema, maeneo ya mpakani katika nchi hizo tatu yamekumbwa na ugaidi wa makundi ya wakufurishaji na kwamba oparesheni hiyo ilianza wiki moja iliyopita.

Hii si mara ya kwanza kwa nchi za ukanda wa Ziwa Chad ambazo ni Niger, Nigeria, Chad na Cameroon, kuanzisha oparesheni dhidi ya kundi la Boko Haram ambalo lilianzisha uasi wake miaka saba iliyopita katika nchi hizo nne.

Tokea Boko Haram ianzishe uasi wake Nigeria mwaka 2009, watu elfu 20 wamepoteza maisha. Aidha zaidi ya watu milioni mbili wamefanywa wakimbizi kufuatia ugaidi wa Boko Haram.

Neno Boko Haram kwa lugha ya Kihausa lina maana ya 'elimu kutoka nchi za Magharibi ni haramu'. Kundi hilo la Boko Haram ambalo lina ufahamu usio sahihi na potovu kuhusu dini ya Kiislamu, limekuwa likitekeleza hujuma katika maeneo mbalimbali ya Nigeria hasa kaskazini mwa nchi hiyo.