-
Al-Azhar yaunga mkono ukarabati wa Gaza bila ya kuondolewa wakazi wake
Feb 13, 2025 23:05Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar nchini Misri kimetoa mwito kuungwa mkono misimamo ya Misri na mataifa mengine ya Kiarabu katika ujenzi na ukarabati mpya wa Ukanda wa Gaza bila ya kuondolewa wakazi wake.
-
OCHA: Mamilioni ya watu wameendelea kutoroka makazi yao nchini DRC
Feb 13, 2025 23:04Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema kuwa, mamilioni ya watu wanaendelea kuyahama makazi yao Kivu Kaskazini na Kivu Kusini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
Viongozi wa kanisa Kongo wakutana na waasi wa M23
Feb 13, 2025 09:05Ujumbe wa taasisi mbili za kanisa nchini Jamhuri wa Kidemokrasi ya Kongo umekutana na waasi wa M23 mashariki mwa taifa hilo katika juhudi za hivi karibuni za kusaka amani na mazungumzo baada ya wiki kadhaa za mapigano.
-
Polisi ya Nigeria yakadhibisha kutoweka maelfu ya bunduki
Feb 13, 2025 07:50Jeshi la Polisi la Nigeria limekanusha ripoti kwamba maelfu ya silaha zimetoweka kwenye maghala yake ya silaha na kuitaja rupoti hiyo kuwa ni ya kupotosha na isiyo sahihi.
-
Wanajeshi wa Ufaransa kuondoka Senegal mwishoni mwa 2025
Feb 13, 2025 07:00Ufaransa na Senegal zimeeleza kuwa zimeamua kuunda tume itakayoafanya maandalizi ya kuondoka wanajeshi wa Ufaransa katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi ifikapo mwisho mwa mwaka huu.
-
Jeshi la Sudan lachukua udhibiti wa kituo kikuu cha wanamgambo wa Rapid Support Forces
Feb 13, 2025 03:21Jeshi la Sudan limetangaza kudhibiti kikamilifu mji wa Jiad, kituo kikuu cha wanamgambo wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) karibu na Khartoum. Mafanikio hayo yanatambuliwa kuwa ni hatua muhimu na ya kimkakati katika njia ya kulinda mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.
-
Msomi wa Misri amshambulia vikali Trump, aitaka Cairo kusimama kidete dhidi ya bwabwaja zake
Feb 13, 2025 03:21Msomi wa Misri amemshambulia vikali Rais Donald Trump wa Marekani na kutoa wito wa kutolewa jibu kali dhidi ya kiongozi huyo akisema: "Lazima tusimame imara na ngangari dhidi ya Trump, na misaada ya Marekani inapaswa kupelekwa kuzimu."
-
Makumi ya wapiganaji wa ISIS wauawa katika mapigano na vikosi vya Puntland, Somalia
Feb 13, 2025 03:20Makumi ya wanamgambo wa ISIS wameuawa katika makabiliano makali na vikosi vya usalama katika eneo linalojitawala la Puntland huko Somalia jana Jumatano, huku vikosi vya usalama vikipata hasara katika mapigano hayo yaliyoanza Jumanne iliyopita.
-
Afrika Kusini: Katu hatutaondoa kesi dhidi ya Israel ICJ licha ya vitisho vya Trump
Feb 12, 2025 23:23Afrika Kusini imeapa kutoondoa kesi yake ya mauaji ya kimbari dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), licha ya vitisho, mashinikizo na kukatiwa misaada na utawala wa Donald Trump.
-
Kongo yapiga marufuku ndege kutoka Rwanda
Feb 12, 2025 23:22Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imefunga anga yake kwa ndege zote za kiraia na za serikali zilizosajiliwa au zile makazi yake nchini Rwanda.