-
Mume wa Rais Samia Suluhu Hassan aaga dunia
Sep 07, 2026 10:29Mume wa Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw.Hafidh Ameir Hassan ameaga dunia hii leo tarehe 07 Septemba, 2026.
-
Uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha moto uliosababisha vifo vya watu 22 harusini, Kinshasa
Sep 06, 2026 11:29Mamlaka husika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimeanzisha uchunguzi kuhusu moto uliotokea kwenye sherehe ya harusi jijini Kinshasa na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 22.
-
Jimbo la Plateau nchini Nigeria lafunga shule kutokana na mlipuko wa Diphtheria
Sep 06, 2026 11:26Serikali ya Jimbo la Plateau linalopatikana kaskazini-kati mwa nchi ya Nigeria imeamuru kufungwa kwa muda usiojulikana shule za serikali na za watu binafsi za msingi na sekondari kuanzia tarehe 7 mwezi huu wa Septemba kutokana na kuenea ugonjwa wa diphtheria katika maeneo manne ya serikali za mitaa katika jimbo hilo.
-
Polisi Kenya yawaonya wanasiasa, yataka notisi za mikutano, maandamano zitolewe siku 3 kabla
Sep 06, 2026 02:59Jeshi la Polisi la Kenya (NPS) limewaonya viongozi wa kisiasa na wafuasi wao kwamba litatekeleza kikamilifu Sheria ya Utulivu wa Umma wakati nchi hiyo inaingia katika kipindi cha kampeni za uchaguzi.
-
Niger: Jaribio la uasi wa jeshi lilichochewa na mtandao mpana ukiongozwa na Ufaransa
Sep 06, 2026 02:57Serikali ya Niger imeishutumu Ufaransa kwa kuchochea shambulio dhidi ya kituo muhimu cha jeshi la anga lililofanywa na wanajeshi walioasi wiki iliyopita.
-
DRC yazindua mpango mpya wa mapambano dhidi ya Ebola, yatafuta msaada wa dola bilioni 1.3
Sep 05, 2026 12:05Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na washirika wake wamezindua siku ya Ijumaa mpango mpya wa sekta mbalimbali wa siku 180 unaolenga kuimarisha juhudi dhidi ya mlipuko wa sasa wa Ebola, huku mahitaji ya fedha yakikadiriwa kufikia dola bilioni 1.3 za Kimarekani.
-
UN yaidhinisha ombi la Afrika la kuichora tena ramani ya dunia, Marekani yapinga
Sep 05, 2026 11:28Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Ijumaa ya Septemba 04 limeidhinisha azimio la kura 164 za ndio na 1 ya hapana, linalolenga kurekebisha namna mabara yanavyoonekana kwenye ramani. Marekani ndiyo nchi pekee iliyopiga kura kulipinga azimio hilo.
-
Gesi ya sumu yaua watu 43 wakati wa wizi wa mafuta nchini Nigeria
Sep 05, 2026 02:57Takriban watu 43 wamefariki dunia baada ya kuvuta gesi yenye sumu wakati wa operesheni haramu ya kuvuta mafuta kwenye bomba katika Jimbo la Rivers, kusini mwa Nigeria.
-
Africa CDC: Ni mapema mno kutangaza mripuko wa Ebola umedhibitiwa DRC
Sep 04, 2026 10:38Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (Africa CDC) vimetangaza kuwa bado ni mapema mno kusema kwamba mripuko wa Ebola huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umedhibitiwa, licha ya kuweko dalili za kupungua sana ugonjwa huo katika wiki za hivi karibuni.
-
WFP yalaani mashambulizi dhidi ya malori ya misaada kusini mwa Sudan
Sep 04, 2026 03:18Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) limetangaza kwamba malori yake mawili yalishambuliwa kutokea angani siku ya Jumapili nje ya eneo la Dilling la Jimbo la Kordofan Kusini, huko kusini mwa Sudan, wakati yalipokuwa njiani kupeleka chakula cha msaada kwa wakimbizi waliokwama kwenye eneo la Kadugli.